1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiGuyana

Moto uliowaua wanafunzi 19 uliwashwa na mwanafunzi

24 Mei 2023

Mwanafunzi alianzisha moto ulioteketeza bweni Guyana kwa sababu ya kunyang'anywa simu.

https://p.dw.com/p/4Rjyi
Schulbrand in Guyana
Picha: Guyana's Department of Public Information/AP Photo/picture alliance

Moto ulioteketeza bweni la shule moja mwishoni mwa wiki na kuwauwa watoto 19 nchini Guyana unaaminika kuanzishwa na mwanafunzi aliyekuwa na hasira kwa sababu ya kunyang'anywa simu yake ya mkononi.

Hayo ni kwa mujibu wa chanzo cha serikali. Mkasa huo wa moto uliotokea Jumapili iliyopita uliteketeza jengo la shule katika mji wa Mahdia, ambalo lilikuwa na wasichana wenye umri wa kati ya miaka 11-17 na 16-17.

Wengine bado wamelazwa hospitali. Ripoti rasmi ya polisi ilithibitisha kuwa mwanafunzi wa kike anashukiwa kwa kuanzisha moto huo kwa sababu simu yake ilichukuliwa.

Chanzo cha serikali kimesema mwanafunzi huyo alikiri kuhusika na shambulizi hilo la moto na yuko chini ya ulinzi wa polisi hospitalini.