1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAsia

Moto mkubwa waunguza ghala la risasi Indonesia

30 Machi 2024

Wazimamoto nchini Indonesia walikuwa wanapambana kuzima moto mkubwa uliozuka Jumamosi kwenye ghala la risasi nje ya mji mkuu Jakarta, na kusababisha milipuko kadhaa na moshi mkubwa angani.

https://p.dw.com/p/4eHNr
Moto Indonesia
Maafisa wamesema hakuna mtu aliekufa katika mlipuko wa moto JakartaPicha: WILLY KURNIAWAN/REUTERS

Hakuna mtu aliyeripotiwa kufariki katika tukio hilo, afisa wa kijeshi Mohammad Hasan aliwaambia waandishi wa habari katika eneo la tukio, akisema moto huo ulizuka katika sehemu ya kituo ambacho kilitumika kuhifadhi risasi zilizokwisha muda wake.

"Tumekagua eneo, na kiongo zake, hakuna vifo," Hasan aliuambia mkutano wa waandishi wa habari karibu na eneo la tukio mjini Bekasi, nje kidogo ya Jakarta.

"Risasi zilizoisha muda wake zina kemikali ambazo zinaweza kutokuwa shwari ... Kunaweza kuwa na misuguano ambayo ilisababisha moto," alisema.

Kanda za video zilizorushwa na mtandao wa ndani wa Kompas TV zinaonyesha miali ya rangi ya chungwa na mawingu ya moshi yakitanda angani usiku, huku milipuko mikubwa ikisikika kutoka umbali wa kilomita kadhaa.

Kuchomwa kwa misitu Indonesia

Soma pia: Indonesia yasimamisha uokoaji baada ya volkano kuripuka tena

Timu za wazima moto na wahudumu wa afya ziilikuwa zinanekana karibu na eneo hilo, lakini hawakuweza kukaribia moto ulipokuwa ukiendelea kuwaka, kulingana na ripoti za vyombo vya habari vya ndani. Walisema moto huo ulianza majira ya saa 10:30 jioni.

Mkazi wa eneo hilo Arga Nanda aliiambia KompasTV kuwa alisikia mlipuko mkubwa ambao ulitikisa milango na madirisha. Watu walikimbilia barabarani wakidhani ni tetemeko la ardhi, alisema.

Afisa wa jeshi Kristomei Sianturi aliiambia chaneli hiyo kwamba mamlaka zilikuwa zinawahamisha watu kutoka vitongoji vya karibu. Wazima moto bado hawakuweza kuzima moto huo, alisema, na kuongeza sababu yake haijajulikana.

Pia aliwaonya wakazi kutogusa vitu vyovyote ambavyo vinaweza "kurushwa" nje na milipuko.

Chanzo: mashirika