1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW-Russia na Umoja wa Ulaya zatiliana saini makubaliano ya kibiashara na ya kisiasa.

11 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFEa

Russia na Umoja wa Ulaya zimetiliana na saini makubaliano ya kuwa na ushirikiano wa karibu katika biashara na masuala ya kisiasa.Rais wa Russia Vladimr Putin,amewaambia waandishi wa habari mjini Moscow,kuwa ana matumaini makubaliano hayo yatasaidia kuundwa kwa Ulaya isiyokabiliwa na mgawanyiko.

Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya,Jose Manuel Barroso ameunga mkono hisia hizo za Rais Putin.

Pande hizo mbili zimekubaliana kuendelea na mazungumzo zaidi yenye lengo la kuondoa vikwazo vilivyopo katika sheria za viza.

Mataifa ya Umoja wa Ulaya kwa hivi sasa yanapakana na Russia tangu Umoja huo ulipopanuka mwaka jana,kwa kuziingiza katika umoja huo nchi kadhaa za Ulaya ya Mashariki.