1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW: Olmert na Putin wajadili mradi wa nyuklia wa Iran

19 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Ec

Waziri Mkuu wa Israel,Ehud Olmert amesema, amehakikishiwa na Rais Vladimir Putin wa Urusi kuwa usalama wa nchi yake,ni kipaumbele cha Urusi.

Olmert alikutana na Putin mjini Moscow kujadili matokeo ya mazungumzo yaliyofanywa na Rais Putin mjini Teheran,kuhusika na mradi wa nyuklia wa Iran.Hapo awali,Putin alizungumza moja kwa moja na umma wa Urusi katika televisheni.Aliitumia fursa hiyo kuionya tena Marekani kuwa Urusi itachukua hatua ikiwa Washington haitotia maanani wasiwasi wa Moscow kuhusika na mpango wa Marekani,kutaka kuweka mitambo ya kinga dhidi ya makombora katika Ulaya ya Mashariki.Putin pia alisema,vita vya Marekani nchini Iraq havielekei kokote na akaashiria kuwa uvamizi huo umeazimia kudhibiti visima vya mafuta nchini Iraq.