1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW : Afisa mwandamizi wa Dagestan auwawa

21 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFBj

Afisa mwandamizi wa serikali katika Jamhuri ya Dagestan nchini Russia ameuwawa.

Zagir Arukhov waziri wa habari na uraia wa Dagestan ameuwawa na mripuko akiwa ngazini nyumbani kwake.Habari zinasema mlinzi wake pia ameuwawa.Dhamira ya mauaji hayo bado haijulikani.

Wachunguzi wa mambo wa Russia wanasema mauaji ya kisiasa huko Dagestan ni jambo la kawaida kutokana na mizozo ya biashara na uhasama wa kiuokoo.