1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoMorocco

Morocco yatishia kususia Kombe la Mataifa, Afrika

29 Desemba 2022

Timu ya taifa ya Morocco imetishia kususia kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani kutokana na mvutano na Algeria.

https://p.dw.com/p/4LWUH
Die besten Momente der Fußball WM 2022 Katar
Picha: Manu Fernandez/AP/picture alliance

Baada ya mafanikio makubwa iliyoyapata kwenye michuano ya Kombe la Dunia, timu ya taifa ya Morocco huenda ikasusia kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani - CHAN itakayofanyika mwezi ujao kutokana na mvutano wa kidiplomasia na mwenyeji wa michuano, Algeria. Shirikisho la Soka la Morocco limesema limeandika barua kwa Umoja wa Afrika likishinikiza timu yake kusafiri moja kwa moja kwa kutumia ndege binafsi ya shirika la Royal Air Maroc kutoka mji mkuu Rabat hadi hadi jiji la Constantine nchini Algeria ambako kutafanyika michuano hiyo.Ndege za jeshi na za kibiashara za nchini Morocco zimezuiwa kupita katika anga ya Algeria tangu majirani hao wawili walipovunja mahusiano ya kidiplomasia mwaka jana, kutokana na masuala kadhaa ambayo ni pamoja na eneo linalozozaniwa la Sahara Magharibi.