1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MONROVIA:Gorge Weah aongoza katika uchaguzi wa urais

15 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CERo

Mchezaji Mpira mashuhuri wa zamani Gorge Weah anaongoza wagombea wengine 21 wa uchaguzi wa Urais nchini Liberia katika matokeo ya uchaguzi wa kwanza kuwahi kufanywa nchini humo tangu kumalizika kwa vita vya kienyeji.

Weah amepata asilimia 30 ya kura hadi kufikia sasa huku

mpinzani wake wa karibu Ellen Johnson Sirleaf mwanamama mchumi wa benki ya dunia akiwa na na asilimia 17 ya kura.

Bado kuna uwezekano wa kufanyika kwa raundi ya pili ya uchaguzi kati ya wagombea wawili watakaobakia kwa sababu Weah hajafikia uwingi wa kura unaohitajiwa kuwa mshindi pekee.

Baraza la usalama la Umoja wa Matifa limeusifu uchaguzi wa Liberia kwa kufanyika kwa njia ya amani.

Baraza hilo limesema hatua hii huenda ikawa muhimu katika kurejesha amani katika taifa hilo lililositisha vita mwaka 2003.