1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Monrovia: Mkuu wa WFP azuru Liberia

13 Novemba 2003
https://p.dw.com/p/CEDt
Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), atatembelea Liberia mwishoni mwa wiki ili kukagua harakti za msaada wa kiutu, katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi iliyobomolewa kwa vita, Umoja wa Mataifa ulisema hii leo. James Moris atakuwa afisa wa ngazi ya juu kabisa wa Umoja wa Mataifa kuizuru nchi hiyo, tangu vilipowekwa vikosi vya kulinda amani mwezi uliopita, ilisema taarifa ya umoja huo. Morris ataonana na Mwenyekiti wa Liberia Gyude Bryant, mfanya biashara aliyeteuliwa katika mwezi wa Oktoba kuiongoza serikali ya mpito hadi ufanyike uchaguzi mwaka 2005, sawa na mjumbe wa Umoja wa Mataifa Jacques Klein na maafisa wengine wa ngazi ya juu, taarifa ilisema.