1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Monrovia. George Weah aongoza .

14 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CES9

Matokeo ya mwanzo katika uchaguzi mkuu wa kwanza baada ya vita nchini Liberia yanaonyesha kuwa mwanasoka maarufu duniani George Weah na waziri wa zamani wa fedha Ellen Johnson-Sirleaf huenda ikabidi kupambana katika duru ya pili ya uchaguzi.

Siku mbili baada ya uchaguzi wa kihistoria uliofanyika siku ya Jumanne wa rais na bunge, matokeo taratibu yanaanza kupatikana katika kura hiyo ambayo ilikuwa na lengo la kuhitimisha mateso ya miaka 14 walioyokabiliana nayo wananchi wa Liberia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Wagombea 22 wamepigiwa kura, na duru ya pili imepangwa kufanyika katika muda wa wiki nne kati ya wagombea wawili waliopata kura nyingi, ama haitafanyika iwapo mgombea mmoja ataweza kupata zaidi ya asilimia 50 ya kura.