1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MONROVIA: Ellen Johnson-Sirleaf aongoza katika uchaguzi wa Liberia

10 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CEJw

Matokeo ya mwanzo ya uchaguzi nchini Liberia yanayonyesha kwamba mwanauchumi wa zamani wa benki ya dunia,, Ellen Johnson-Sirleaf, anaongoza. Tume ya uchaguzi nchini humo imesema Johnson Sirleaf anaongoza kwa asilimia 56 katika kura zote zilizohesabiwa kutoka thuluthi mbili ya vituo vyote vya kupigia kura.

Mpinzani wake katika uchaguzi huo wa marudio, mwanasoka mashuhuri George Weah, amejipatia asilimia 44. kiongozi wa tume ya kulind amani ya umoja wa mataifa nchini Liberia amesema uchaguzi huo ulifanyika kwa amani na haukuwa na udanganyifu. Matokeo kamili kamili yanatarajiwa kutangazwa hivi karibuni.