1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MONROVIA. Bibi Ellen Johnson-Sirleaf anatarajiwa kunyakua urais wa Liberia

11 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CEJV

Bibi Ellen Johnson Sirleaf mwanauchumi wa zamani wa Benki ya dunia na aliyekuwa waziri wa fedha nchini Liberia anatazamiwa kuwa kiongozi wa kwanza mwanamke baada ya matokeo ya asilimia 90 ya kura zilizohesabiwa kuonyesha anaongoza.

Tume ya uchaguzi ya Liberia imesema matokeop hayo yanaonsesha kuwa bibi Ellen Johnson amepata zaidi ya asilimia 55 huku mpinzani wake George Weah akiwa na asilimia 42.

Bwana George Weah mwanasoka maarufu wa zamani amewasilisha malalamiko yake kwa tume ya uchaguzi kuwa uchaguzi huo ilikumbwa na udanganyifu.

Muwakilishi wa umoja wa mataifa nchini Liberia amesema kwamba uchaguzi huo haukukumbwa na vurugu na pia ulikuwa wa uwazi.