1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Modi kuelekea Moscow

5 Julai 2024

Ikulu ya Kremlin inasema Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi, ataitembelea Urusi Jumatatu ijayo kwa mazungumzo na Rais Vladimir Putin.

https://p.dw.com/p/4htDk
 Mumbai 2024 |  Narendra Modi
Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi.Picha: Punit Paranjpe/AFP/Getty Images

Awali ziara hiyo ilitangazwa na maafisa wa Urusi mwezi uliopita lakini hawakuwa wamebainisha tarehe ya kufanyika kwake.

Urusi ina mafungamano mazuri na India tangu enzi za Vita Baridi na umuhimu wa New Delhi kama mshirika mkubwa wa kibiashara umeongezeka tangu kuanza kwa vita vya Ukraine.

Soma zaidi: Rais wa halmashauri kuu EU akutana na waziri mkuu India Narendra Modi

China na India zimekuwa wanunuzi wakubwa wa mafuta ya Urusi kufuatia vikwazo vya Marekani dhidi ya Moscow na washirika wake wa Magharibi.

Chini ya uongozi wa Modi, India imekwepa kuikosowa Urusi kwa uvamizi wake dhidi ya Ukraine, huku ikisisitiza haja ya kupatikana suluhisho kwa njia za amani.