1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Modi afunguwa hekalu nyumbani kwa mungu wa Kihindu

22 Januari 2024

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi amefuguwa hekalu kubwa kabisa la mungu wa madhehebu ya Kihindu, Lord Ram, katika mji wa Ayodhya, eneo linaloaminika kuwa ndiko alikozaliwa mungu huyo.

https://p.dw.com/p/4bWsw
Narendra Modi
Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi, kwenye uzinduzi wa Hekalu la Lord Ram.Picha: Rajesh Kumar Singh/AP Photo/picture alliance

Hata hivyo, hekalu hilo limejengwa kwenye ardhi ambako kwa miongo mingi kulikuwa na msikiti kabla ya kuvunjwa na Wahindu wenye misimamo mikali miaka ya 1990, na kuibua machafuko makubwa.

Modi amejaribu kuelezea hatua hiyo kuwa ni jaribio la kuleta maridhiano, huku kukiwa na mashaka kwamba uzinduzi huo utaibua mgawanyiko ndani ya India. 

Hekalu hilo ni sehemu ya ahadi muhimu 35 za chama cha Modi cha BJP, lakini limekuwa suala tata la kisiasa lililochangia kupunguza umaarufu na mamlaka ya chama hicho.