1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mnangagwa atangazwa mshindi wa urais Zimbabwe

Sylvia Mwehozi
3 Agosti 2018

Tume ya uchaguzi  Zimbabwe imemtangaza Emmerson Mnangagwa mshirika wa zamani wa Robert Mugabe kuwa mshindi wa  kinyan'ganyiro cha  urais katika  uchaguzi uliofanyika Jumatatu wiki hii.

https://p.dw.com/p/32ZIb
Simbabwe Wahl | Emmerson Mnangagwa, Präsident
Picha: picture-alliance/Photoshot/S. Jusa

Tume ya uchaguzi  Zimbabwe imemtangaza Emmerson Mnangagwa mshirika wa zamani wa Robert Mugabe kuwa mshindi wa  kinyan'ganyiro cha  urais katika  uchaguzi uliofanyika Jumatatu wiki hii. Kwa mujibu wa matokeo hayo Mnangagwa ameshinda baada ya kujipatia asilimia 50.8 ya kura akimshinda Nelson Chamisa wa chama cha upinzani MDC aliyepata asilimia 44.3 ya kura na hivyo tume ya uchaguzi kumtangaza rasmi Mnangagwa kuwa mshindi wa nafasi ya urais.  Katika ujumbe wake kupitia ukurasa wa Twitter Mnangagwa aliwashukuru  wa Zimbabwe kwa kumchagua kushika nafasi hiyo na kusema huu sasa ni mwanzo mpya.  Ili kutangazwa mshindi wa nafasi ya urais mgombea anatakiwa kupata zaidi ya asilimia 50 ya kura. Mgombea wa chama cha upinzani MDC alifanya vizuri katika maeneo ya mjini wakati Mnangagwa alipata kura nyingi vijijini. Hayo yanajiri mnamo wakati watu sita wakifariki dunia kufuatia mapambano kati ya waandamanaji wa upinzani na askari mjini Harare.