1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mmoja aswekwa rumande njama za kushambulia kanisa Ujerumani

27 Desemba 2023

Polisi nchini Ujerumani imesema imemweka rumande mwanaume mmoja anayeshukiwa kupanga njama za kufanya shambulio kwenye kanisa kuu mjini Cologne wakati wa mkesha wa mwaka mpya.

https://p.dw.com/p/4abEx
Kanisa Kuu mjini Cologne likionekana kwa mbali kutokea kingo za mto Rhein.
Kanisa Kuu mjini Cologne (jengo la kale lenye minara miwili) ni moja ya alama muhimu nchini Ujerumani. Picha: Horst Galuschka/IMAGO

Siku ya Jumapili polisi iliwakamata jumla ya wanaume watano kwenye mji wa Wesel kiasi umbali wa kilometa 100 kutoka mji wa Cologne kuhusiana na njama ya kulilenga kanisa hilo.

Hata hivyo hapo jana wanne kati yao waliachiwa huru  na polisi imesema mmoja atabakia rumande kama sehemu ya hatua muhimu ya "kuepusha kutokea balaa". Hati ya mahakama imetoa kibali kwa mwanaume huyo aliyetambulishwa kwa jina moja la Tajik kuwekwa kizuizi hadi mnamo Januari 7.

Polisi imesema inatumia njia zote zilizopo kuepusha kutokea kisa chenye madhara kwa umma na kulilinda kanisa la mjini Cologne ambalo ni moja ya majengo ya kale kabisa barani Ulaya na tunu nchini Ujerumani.