1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Wagner: Vita nchini Ukraine vinaweza kudumu kwa miaka kadhaa

12 Februari 2023

Mmiliki wa Kikundi cha Mamluki wa Urusi cha Wagner Yevgeny Prigozhin amesema vita nchini Ukraine vinaweza kudumu kwa miaka kadhaa.

https://p.dw.com/p/4NNqH
Russland Wagner-Chef Jewgenij Prigoschin
Picha: Mikhail Metzel/TASS/IMAGO

Prigozhin amesema vita hivyo vinaweza kudumu kwa miezi 18 hadi miaka miwili ili kuiwezesha Urusi kuchukua udhibiti kamili wa eneo la mashariki mwa Ukraine la Donbas. 

Prigozhin ambaye mamluki wake wa Wagner wamekuwa mstari wa mbele katika uvamizi huo ameendelea kuwa vita hivyo vinaweza kuendelea hadi miaka mitatu ikiwa Urusi itaamua kuchukua udhibiti wa maeneo mapana zaidi mashariki mwa mto Dnieper.

Kauli ya milionea huyo ambaye ana uhusiano wa karibu na Rais Vladimir Putin imedhihirisha wazi matatizo ambayo jeshi la Urusi linakabiliana nayo katika uwanja wa vita, ambapo awali Moscow ilitarajia kuvimaliza vita hivi ndani ya wiki chache ilipoamua kuivamia Ukraine  Februari 24, mwaka jana.