1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiBurundi

Mkuu wa Shirika la Wakimbizi kukutana na wakimbizi wa Kongo

9 Februari 2023

Mkuu wa Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR, Philippe Grandi, ziarani nchini Burundi kuzitembelea kambi za wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

https://p.dw.com/p/4NIBD
Burundi Refugees Flüchtlingscamp
Picha: YASUYOSHI CHIBA/AFP via Getty Images

Mkuu huyo wa UNHCR amesema mazungumzo yake ya ana kwa ana Rais Evariste Ndayishimiye yametuwama juu ya swala la wakimbizi zaidi ya elfu 80 kutoka nchi jirani ya Kongo.

Grandi  amesma kuna umuhimu Burundi kujengewa uwezo zaidi ili iwafanyinye iwahudumie vizuri zaidi wakimbizi hao.

"Kunahitajika Burundi kupewa uwezo zaidi, ili wakimbizi wanaopokewa waweze kuishi katika mazingira ya kiutu, pia wakimbizi wapewe uwezo wa kujiajiri ili wasitegemee tu misaada ya kibinaadamu. Tuna imani Burundi itawahudumia ipasavyo wakimbizi kutoka Kongo, kwani Warundi wanao uzoefu wa maswala ya ukimbizi." alisema Grandi.

Kabla ya hapo mkuu huyo wa UNHCR alikutana kwa mazungumzo na mawaziri wa mambo ya kigeni na yule wa mambo ya ndani, maendeleo ya jamii na usalama, Martin Niteretse, anayehusika na maswala ya wakimbizi.

Burundi yaendelea kupokea wakimbizi kutoka Kongo

Waziri Niteretse amemwambia Grandi kwamba katika jumla ya wakimbizi elfu 88 walio Burundi, asilimia 99 ni kutoka nchi jirani ya Kongo. Waziri huyo ameongeza kuwa machafuko yanayoendelea katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo hupelekea wakimbizi kuzidi kukimbilia Burundi.

"Kambi 5 ziliopo zimefurika, kunahitajika uwezo wa kifedha ili kuwekwe kambi nyingine ya 6 itakayowapa hifadhi wakimbizi kutoka Kongo. Eneo tayari tumeliandaa katika tarafa ya Giharo mkoani Rutana kusini mashariki."

''Kuikumbusha dunia umuhimu wa kuiunga mkono Burundi''

Äthiopien Konflikt in Tigray | Flüchtlinge in Sudan
Picha: Ashraf Shazly/AFP/Getty Images

Kwa upande wake, Mkuu wa UNCHR ameahidi kuunga mkono juhudi za Burundi katika kuwapokea wakimbizi wapya

"Ndilo lengo la ziara yangu hapa, kuikumbusha dunia umuhimu wa kuiunga mkono Burundi, kutakuwa na manufaa kwa Burundi, nchi za kanda hii na bara ziama la Afrika. Utakuwa ni ujumbe wenye nguvu nitakaoendelea kuutowa."

Baada ya mazungmzo yake na viongozi wa serikali, mkuu huyo wa UNHCR anatarajiwa kuzitembelea kambi zilizowapokea wakimbizi kutoka Kongo, ikiwa ni pamoja na  Kinama Muyinga, Musasa katika mkoa wa Ngozi, Kavumu mkoani Cankuzo, Bwagirizwa na Nyankanda katika mkoa wa Ruyigi, mashariki mwa Burundi.

Pia mkuu huyo wa UNHCR amefurahishwa kuona wakimbizi zaidi ya laki mbili wa Burundi tayari wamerejea nchini kutoka nchi za Tanzania, Rwanda, Kongo na Kenya.