Mkuu wa polisi Lebanon aapa kukabiliana na wanaoitishia nchi yake
26 Januari 2008BEIRUT:
Mkuu wa kikosi cha Polisi cha Lebanon ameapa kukabiliana na wale aliowaita wanaoitishia nchi yake.Mkuu huyo alikuwa anazungumza wakati wa ibada ya wafu kwa heshima ya afisa wa polisi alieuliwa na bomu mjini Beirut.Captain Wisan Eid, ambae alisaidia kuchunguza mauaji yanayofanyika nchini humo, aliuliwa wakati bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari, kulipuka jana Ijumaa, katika mtaa wa wakristo wa Beirut.Watu wengine watano waliuawa na 42 kuwajeruhi katika shambulio hilo.Mauaji ya Eid ndio mapya katika misururu ya mauaji ya kisiasa ambayo yameikumba Lebanon kwa kipindi cha miaka mitatu sasa. Mvutano kati ya watu wanaounga mkono Syria dhidi ya wanaoipinga umeifanya nchi hiyo kutokuwa na rais kwa mda wa miezi miwili kufuatia kumalizika kwa muhula wa Emile Lahoud.Lahoud anaegemea Syria.