1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkuu wa NATO aonya dhidi ya kuigawanya Marekani na Ulaya

15 Februari 2024

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami - NATO Jens Stoltenberg amezionya nchi wanachama dhidi ya kuruhusu kuingizwa kwenye mpasuko kati ya Marekani na Ulaya

https://p.dw.com/p/4cRwA
NATO | Jens Stoltenberg
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami - NATO Jens StoltenbergPicha: Virginia Mayo/AP/picture alliance

Hayo ni wakati wasiwasi ukiendela kuongezeka juu ya kujitolea kwa Marekani kwa washirika wake ikiwa Donjald Trump atarejea madarakani. Stoltenberg ametoa kauli hiyo kwenye mkutano wa mawaziri wa ulinzi wa NATO uliofanyika hivi leo mjini Brussels. 

Katibu Mkuu huyo wa NATO, amesema anakaribisha hatua ya washirika wa Ulaya kuwekeza zaidi katika masuala ya ulinzi na NATO imekuwa ikitaka hivyo kwa miaka mingi.

Stoltenberg aidha amesema hiyo ndiyo njia ya kuimarisha muungano huo wa ulinzi na akaonya dhidi ya kuchukua mkondo unaoashiria wanajaribu kuitenga Ulaya na Amerika Kaskazini.

Soma pia:Stoltenberg aonya dhidi ya kuigawa Marekani na Ulaya

Huku wakikabiliwa na vita vya Ukraine ambavyo vimesababisha shinikizo kubwa kwa raslimali za kijeshi na fedha, na msaada wa Marekani ukikabiliwa na mvutano katika bunge la Congeress, viongozi wa Ulaya na maafisa wa ngazi za juu wametahadharisha kwamba Ulaya sharti iwekeze zaidi katika majeshi yake na teknolojia mpya, na kuongeza utengenezaji wa silaha.