1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkuu wa Mkoa aamuru kukamatwa kwa kijiji kizima hiko Mbeya

Sylvia Mwehozi
17 Agosti 2018

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Albert Chalamila ametoa agizo la kukamatwa wanakijiji wote wa kijiji cha Ngole kata ya Ilunga jijini Mbeya kwa madai ya uharibifu wa miundombinu ya maji.

https://p.dw.com/p/33Ihf

Hata hivyo inadaiwa kuwa mkasa huo umechochewa na mgogoro wa ardhi uliokuwapo kwa muda mrefu. Sylvia Mwehozi amezungumza na diwani wa kata ya Ilunga Christopher Njerenje, wilaya ya Mbeya ambae kwanza anaanza kwa kuelezea kisa na mkasa cha kutolewa agizo la mkuu wa mkoa la kukamatwa kijiji kizima na kama agizo hilo limeanza kutekelezwa.