1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaThailand

Mkuu wa majeshi nchini Thailand aahidi kutofanya mapinduzi

12 Mei 2023

Mkuu wa majeshi nchini Thailand ameahidi kutofanya mapinduzi wakati vyama vya kisiasa nchini humo vikijiandaa kukamilisha kampeini ya uchaguzi leo Ijumaa kabla ya uchaguzi

https://p.dw.com/p/4RHe6
Thailand | Prayuth Chan-ocha
Picha: Sakchai Lalit/AP Photo/picture alliance

Uchaguzi huo huenda ukashuhudia serikali ya sasa inayoungwa mkono na jeshi ikiondolewa madarakani na wapiga kura. Jenerali Narongpan Jitkaewthae ametoa ahadi hiyo licha ya jeshi kuonekana likinyakuwa kwa nguvu madaraka mara kadhaa nchini Thailand katika kipindi cha karne moja iliyopita.

Soma zaidi:Waziri Mkuu wa Thailand atangaza uchaguzi mkuu kufanyika Mei

Inabashiriwa kwamba wapiga kura nchini humo huenda wakakafanya maamuzi ya kuiondowa serikali inayoshikiliwa na mkuu wa zamani wa jeshi na kiongozi wa mapinduzi waziri mkuu Prayut Chan-O-Cha. Hatua hiyo imeongeza khofu kwamba jeshi huenda likapambana kutaka kubakia madarakani. Uchaguzi utafanyika Jumapili ukiwa ni mpambano kati ya kiongozi wa upinzani wa chama cha Pheu Thai ambaye ni binti wa waziri mkuu wa zamani  Thaksin Shinawatra na waziri mkuu wa sasa anayeungwa mkono na jeshi.