1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
TeknolojiaMarekani

Mkuu wa IMF asema AI ina hatari na mazuri kiuchumi

15 Januari 2024

Mkuu wa shirika la fedha la kimataifa - IMF Kristalina Georgieva amesema teknolojia ya Akili ya kubuni yaani AI inahatarisha upatikanaji wa kazi kote ulimwenguni.

https://p.dw.com/p/4bGIP
Mkuu wa shirika la fedha la kimataifa - IMF Kristalina Georgieva
Mkuu wa shirika la fedha la kimataifa - IMF Kristalina Georgieva Picha: Britta Pedersen/dpa/picture alliance

Georgieva amesema pia teknolojia hiyo inatoa fursa kubwa ya kuimarisha viwango vya uzalishaji na kuchochea ukuaji kimataifa.

Mkurugenzi huyo mkuu wa IMF amesema teknolojia ya AI itaathiri asilimia 60 ya kazi katika nchi zilizoendelea kiuchumi.

Hata hivyo, ripoti ya IMF iliyochapishwa Jumapili usiku inabainisha kuwa ni nusu tu ya ajira zilizoathiriwa na Akili Bunifu, ndizo zitakazoathiriwa kwa njia hasi, na zinazobaki huenda zikanufaika na kuimarika kwa uzalishaji kutokana na AI.

Georgiova amesema lazima ulimwengu uangazie katika kuzisaidia nchi za kipato cha chini kuchangamkia fursa zinazopatikana na teknolojia ya Akili Bunifu.