1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Mkuu wa IAEA kuelekea Urusi kwa mazungumzo kuhusu Ukraine

9 Februari 2023

Rafael Grossi, anatarajiwa kuwasili mjini Moscow leo Alhamisi kwa mazungumzo kuhusu usalama wa nyuklia nchini Ukraine huku mapigano yakiendelea.

https://p.dw.com/p/4NIh0
Rafael Grossi | IAEO Direktor | Pressekonferenz UNO in New York
Picha: Luiz Rampelotto/ZUMA Wire/IMAGO

Hayo yamefahamishwa na Naibu waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Ryabkov aliyesema kuwa ziara ya Grossi ni muhimu ili kufikia makubaliano ya eneo salama lisilohusishwa na vita, lakini akabaini kuwa mazungumzo hayo hayatokuwa rahisi.

Maeneo yenye mitambo ya nyuklia yamekuwa tishio katika kipindi chote cha mzozo wa takriban mwaka mmoja nchini Ukraine, huku mashambulizi karibu na vituo kadhaa ikiwemo kile cha Zaporizhzhia yakizua hofu ya kutokea kwa tukio baya zaidi la nyuklia.