1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkuu wa EU asema mahusiano yanaimarika na Ethiopia

4 Aprili 2023

Mkuu wa sera za kigeni wa umoja wa Ulaya Josep Borell amesema umoja huo unafuatilia mchakato wa usuluhishi wa mzozo katika eneo la Tigray kaskazini mwa Ethiopia

https://p.dw.com/p/4PfpZ
Josep Borrell, Hoher Vertreter der EU für Außen- und Sicherheitspolitik
Picha: picture alliance / ASSOCIATED PRESS

Mkuu wa sera za kigeni wa umoja wa Ulaya Josep Borell amesema umoja huo unafuatilia mchakato wa usuluhishi wa mzozo katika eneo la Tigray kaskazini mwa Ethiopia na utarejesha mahusiano yake ya kawaida na mamlaka za eneo hilo hatua kwa hatua.

Borell amesema leo kwamba ujumbe kwa serikali ya Ethiopia na viongozi wa Tigray ni kuwafanya waelewe kwamba Umoja wa Ulaya unawaangalia jinsi wanavyofanya kuutafutia ufumbuzi mzozo kati yao na umoja huo utarejesha mahusiano pole pole hatua kwa hatua.