1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa umoja wa mataifa kuhusu silaha ndogo ndogo umemalizika bila ya maafikiano

8 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG9V

Mkutano wa Umoja wa mataifa wa kupambana na biashara haramu ya silaha ndogo ndogo haujaleta tija.Wajumbe wameshindwa kuafikiana juu ya waraka wa mwisho wa mkutano huo uliofanyika mjini New-York.Wawakilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali NGO’S yanayabebesha dhamana ,nchi mfano wa India,Iran,Cuba na Pakistan ya kushindwa mkutano huo .Mkutano huo wa wiki mbili ulilenga kutathmini hali ya mambo namna ilivyo,kulinganisha na mkakati uliokubaliwa mwaka 2001 kuhusu biashara ya silaha ndogo ndogo.Biashara jumla ya silaha kama hizo inakadiriwa kufikia dala bilioni nne kwa mwaka.