1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUswisi

Mkutano wa uchumi wa dunia waanza mjini Davos

17 Januari 2023

Mkutano wa Jukwaa la Dunia la Uchumi umeanza leo mjini Davos, Uswisi, huku vita vya Ukraine na mdororo wa uchumi duniani zikiwa mada kuu za mazungumzo.

https://p.dw.com/p/4MILk
WWF Davos 2023 Auftakt/Protest
Picha: Arnd Wiegmann/REUTERS

Baada ya hotuba ya ufunguzi iliyotolewa na mwanzilishi wa jukwaa hilo, Klaus Schwab, macho na masikio vinaelekezwa kwenye hotoba ya Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen, wakati Ulaya ikikabiliwa na mkururo wa changamoto zikiwemo athari za uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine, na machungu yatokanayo mfumuko wa bei na ukuaji hafifu wa uchumi.

Soma pia: Pengo la usawa wa uchumi kijinsia kuzibwa baada ya miaka 257

Mke wa Rais Volodymyr Zelenskiy wa Ukraine, Olena Zelenska, ni miongoni mwa watu wengine watakaolihutubia jukwaa hilo. Katika ripoti yake ya mwaka juu ya hali ya uchumi wa dunia, Jukwaa la Dunia la Uchumi limesema kupanda kwa gharama ya maisha na mizozo ya nishati na chakula ndivyo vizingiti vikuu kwa wakati huu.