1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa mazingira Katowice wakaribia kufikia tamati

Sekione Kitojo
11 Desemba 2018

Mazungumzo yanayopigiwa upatu kuwa muhimu ya mkutano wa Umoja wa mataifa tangu makubaliano ya Paris mwaka 2015 kuhusiana  na mabadiliko ya tabia nchi yamo katika wiki ya mwisho muhimu mjini Katowice,mji mkuu wa Poland.

https://p.dw.com/p/39t8E
Polen COP24 Klimakonferenz in Kattowitz
Picha: picture-alliance/NurPhoto/B. Zawrzel

Lengo  ni  kufikia  muda  uliopangwa  wa  mwishoni  mwa mwaka  katika  kupatikana  makubaliano  ya  utaratibu  juu  ya  vipi kuchukua  hatua  za  kupunguza  zaidi  hali  ya  ongezeko  la  joto duniani. 

Polen COP24 Klimakonferenz in Kattowitz (Imago/ZUMA Press(B. Zawrzel)
Wajumbe wa majadiliano katika mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mazingira nchini Poland 2018Picha: Imago/ZUMA Press(B. Zawrzel

Mawaziri  na  wakuu  wa  nchi  kutoka karibu  nchi 130 wamekuwa wakiwasili  na  wataanza  kutoa  hotuba za  ufunguzi  jioni  ya  leo. Wakati  huo  huo , vikosi  vyao  vya  majadiliano  vinafanyakazi  kwa faragha kuwezesha  kuandika  mswada juu  ya  sheria  kwa  ajili  ya utekelezaji  wa  makubaliano  ya  Paris ifikapo  jioni leo. Jana  waziri mkuu wa  zaani wa  Ufaransa  Ufaransa  Laurent Fabius , ambaye aliongoza  makubaliano  ya  Paris mwaka  2015, alisema atashangazwa  iwapo  hakutapatikana  makubaliano kuhusiana  na utaratibu  utakaofuatwa  ifikapo  mwishoni  mwa  wiki  lakini  kiwango cha  hamasa  ni  suala linalotia  shaka.

"Kutokana  na  ripoti  za  hivi  karibuni  za  kisayansi ambazo zimepatikana, tarakimu  ni  mbaya  na  hatupo  katika  njia  sahihi, kwa  hiyo  tunapashwa  kuwa  na  dhamira  zaidi. hapo  ndio majadiliano  yatatoa  matunda  ama  la  katika  dakika  za  mwisho," amewaambia  waandishi  habari.

Polen COP24 UN-Klimakonferenz in Katowice 2018
Wajumbe wa mkutano wa mazingira wa Umoja wa Mataifa mjini Katowice 2018Picha: DW/I. Banos Ruiz

Taifa  la  kisiwani  katika  bahari  ya  Pasifiki  la  Vanuantu limetoa wito  wa kuundwa  kwa  mfuko mpya  wa "hasara  na  uharibifu" kuhakikisdha  malipo  kutoka  mataifa  tajiri, na  yenye  viwanda , kwenda   katika  mataifa  yale  yaliyoathirika  zaidi  na  maafa ya mazingira.

Ushirika  utasaidia kupunguza  ujoto

Joto  la  wastani duniani linaelekea  kupindukia  lengo kuu lililowekwa katika  makubaliano  ya  Paris  mwaka  2015  la  kupunguza  ujoto duniani, uchunguzi  umeonesha  leo Jumanne. Mwakilishi  maalum wa China  katika  mkutano  wa  Katowice Xie Zhenhua ushirikiano wa mataifa utasaidia kupunguza  ujoto duniani.

"Ushirikiano wa  dunia  katika  nishati  utasaidia  kuondokana  na matumizi ya  nishati  ya  mafuta  na  mkaa na  kuanza  kutumia nishati  salama, na  hii  itakuwa hatua  muhimu  katika  kutatua matatizo  ya  utoaji wa  gesi  za  kaboni na  kuweza  kufikia  lengo  la kudhibiti ujoto  kufikia  nyuzi joto 2 na  hata 1.5."

Polen COP24 UN-Klimakonferenz in Katowice 2018
Mwanaharakati katika mkutano wa mazingira wa Katowice akionya kuhusu matumizi ya nishati ya mafutaPicha: DW/I. Banos Ruiz

Lakini ongezeko  hilo  ifikapo mwishoni  mwa  karne  hii  huenda ikawa  chini  ya  kiwango  cha  juu  mno  kuliko  inavyotarajiwa kutokana  na  juhudi  maalum zinazofanywa  na  baadhi  ya  mataifa kupambana  na  mabadiliko  ya  tabia  nchi, imesema  ripoti  ya hatua  za  kufuatilia  mabadiliko  ya  tabia  nchi , iliyoandikwa  na kundi  la  makundi  huru  matatu  yanayofanya  utafiti   katika  bara  la Ulaya.

Makubaliano  ya  Paris  yanalenga kuzuwia  ongezeko  la  ujoto kufikia  chini  ya  nyuzi  joto mbili  katika  kipimo  cha  Celsius juu  ya enzi  za  kabla  ya  viwanda.

Mwandishi: Sekione  Kitojo / rtre

Mhariri: Josephat  Charo