1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfrika Kusini

Mkutano wa kilele wa kundi la BRICS waingia siku ya pili

23 Agosti 2023

Mkutano wa kilele wa kundi la mataifa yanayoendelea kwa kasi duniani la BRICS, leo unaingia siku ya pili itakayotawaliwa na mjadala muhimu wa kutanua ukubwa wa kundi hilo kwa kuyakaribisha mataifa mengine kuwa wanachama.

https://p.dw.com/p/4VSvX
Mkutano wa Kilele wa BRICS
Mkutano wa Kilele wa BRICS ulianza siku ya Jumanne ya Agosti 22,2023, mjini Johannesburg, Afrika Kusini.Picha: Jerome Delay/AP Photo/picture alliance

Katika siku ya kwanza ya mkutano huo unaofanyika mjini Johannesburg, Afrika Kusini, viongozi wa mataifa hayo ya Brazil, China, India, Afrika Kusini na Urusi, walitoa hotuba zilizomulika mwelekeo wa kundi hilo la kiuchumi na nafasi yake katika ulimwengu wa sasa.

Rais Vladimir Putin wa Urusi ambaye alihutubia jukwaa hilo kwa njia ya mtandao, alisema kundi hilo limepiga hatua katika utekelezaji wa dhamira yake ya kuachana na utegemezi wa dola ya Marekani katika biashara na uchumi.

Hotuba za viongozi wengine ikiwemo rais Xi Jinping wa China, ziligusia umuhimu wa kuimarisha nafasi ya kundi la BRICS kwenye Jukwaa la Kimataifa.