1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa kilele wa Jumuiya ya madola umefunguliwa rasmi

24 Juni 2022

Mkutano wa kilele wa Jumuiya ya madola umefunguliwa rasmi mjini Kigali.

https://p.dw.com/p/4DBHe
Ruanda Kigali | Commonwealth Gipfeltreffen CHOGM
Picha: Luke Dray/Getty Images

Viongozi kadhaa wamezungumza katika hafla ya ufunguzi wa mkutano huo, akiwemo mwenyeji, rais wa Rwanda Paul Kagame, mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya ya Madola, Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson pamoja na Mwanamfalme Charles wa Uingereza anayemwakilisha mama yake, Malkia Elizabeth ambaye ndiye mkuu wa Jumuiya ya Madola.

Mkutano wa kilele wa viongozi wa Jumuiya ya Madola unaanza leo nchini Rwanda huku taifa hilo likichunguzwa kuhusu rekodi yake ya haki za binadamu wakati makubaliano yake ya wahamiaji na Uingereza yakitishia kuangaziwa zaidi katika mkutano huo.

Ushindani mkali wa uongozi wa jumuiya hiyo yenye mataifa 54 ambayo ni makoloni ya zamani ya Uingereza pia unafanyika huku jumuiya hiyo ikikabiliana na mabadiliko ya utambulisho wake na umuhimu wake katika siku zijazo.

Mwanamfalme Charles, anayemwakilisha Malkia Elizabeth II kama mkuu wa Jumuiya ya Madola, amefanya ziara ya kwanza ya kifalme ya Uingereza nchini Rwanda kwa mkutano huo, ambao unakamilika baada ya siku mbili za mikutano ya uongozi.

Mwanamfalme Charles pia anatarajiwa kukutana leo na Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson pembezoni mwa mkutano huo ambaye amekuwa akipigia debe mpango wake uliokosolewa vikali wa kuwahamisha wahamiaji kuelekea Rwanda tangu alipowasili mjini Kigali hapo jana.