1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Viongozi wa Afrika na Korea kusini wajadili maendeleo

4 Juni 2024

Viongozi kadhaa wa kiafrika wanahudhuria hii leo mkutano wa kilele ulioandaliwa na Korea Kusini na ambao umewajumuisha wajumbe kutoka nchi 48 wakiwamo wakuu wa nchi wapatao 30.

https://p.dw.com/p/4gdoX
Soeul, Korea Kusini | Angola | Yoon Suk Yeol na Joao Lourenco
Rais Yoon Suk Yeol wa Korea Kusini akiwa na mwenzake wa Angola Joao Lourenco.Picha: Yonhap/picture alliance

Rais wa Mauritania na mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Mohamed Ould El-Ghazouani amesema wanafurahishwa na msaada wa maendeleo uliotolewa na Korea Kusini.

"Tunafurahia uamuzi huu wa Korea Kusini wa kutoa msaada wa maendeleo wa hadi dola bilioni 10 ifikapo mwaka 2030, ikiwa ni kiwango mara mbili ya kile cha awali, na pia kutenga dola milioni 14 kwa ajili ya uwekezaji wenye tija katika sekta muhimu kama vile biashara, teknolojia, nishati, usalama wa chakula, rasilimali watu na miundombinu."

Soma pia:Korea Kusini kuongeza ushirikiano wake na mataifa ya Afrika

Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol amesema nchi yake inalenga pia kutatanua ushirikiano na Afrika hasa katika sekta muhimu za madini na teknolojia.