1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa jumuiya ya BRICS waanza mjini Johannesburg

22 Agosti 2023

Viongozi wa nchi zinazoinukia kiuchumi BRICS wanakutana mjini Johannesburg kwenye mkutano wa kilele wa 15 wa kundi hilo unaoanza hii leo.

https://p.dw.com/p/4VRMW
Wajumbe kutoka nchi zaidi ya 70 wanahudhuria mkutano huo utakaofanyika hadi Alhamisi.
Wajumbe kutoka nchi zaidi ya 70 wanahudhuria mkutano huo utakaofanyika hadi Alhamisi.Picha: Gianluigi Guercia/AFP/Getty Images

Pamoja na masuala mengine watajadili uwezekano wa kuongeza wanachama na njia za kukabiliana na vikwazo.

Nchi zipatazo 23 zimeomba kujiunga na kundi hilo la nchi tano ambazo ni Afrika Kusini, Brazil,China India na Urusi.

Nchi zinazoomba kujiunga na kundi hilo ni pamoja na Saudi Arabia, Indonesia, Iran, Argentina na Ethiopia.

Hata hivyo India imeonyesha mashaka juu ya mpango huo.

Wajumbe kutoka nchi zaidi ya 70 wanahudhuria mkutano huo utakaofanyika hadi Alhamisi.

Rais wa Urusi Vladimir Putin atajiunga na mkutano huo kwa njia ya video kuepuka amri ya kukamatwa iliyotolewa na mahakama ya kimataifa ya mjini the Hague.

Mahakama hiyo inamtuhumu kwa kuhusika na uhalifu wa kivita nchini Ukraine.