1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa G20 wamalizika bila makubaliano

25 Februari 2023

Mkutano wa viongozi wa sekta ya fedha wa kundi la nchi tajiri na zile zinazoinukia kiuchumi G20, umemalizika bila ya makubaliano ya pamoja huku Urusi na China zikipinga maelezo ya vita vya Ukraine.

https://p.dw.com/p/4NyjK
Indien | Treffen der Finanzminister und Notenbankchefs der G20
Picha: India's Press Information Bureau/via REUTERS

Mkutano huo uliofanyika India umetoa taarifa kwamba hakuna kilichokubaliwa kuhusiana na mgogoro wa Ukraine.  

Viongozi wa kundi la nchi saba tajiri duniani, G7 walitangaza vikwazo vipya hapo jana dhidi ya Urusi wakati mkutano wa G20 ukiendelea katika mji maarufu kwa teknolojia wa Bengaluru nchini India. 

Mawaziri wa nje wa G20 kuanza mazungumzo, Bali

Waziri wa fedha wa Marekani Janet Yellen alikosoa vikali vita vya Urusi Ukraine alivyoviita haramu huku akitaka mataifa ya G20 kuweka juhudi zaidi za kuisaidia Ukraine kupambana na uvamizi wa Urusi. 

Marekani na washirika wake wa viongozi wa kundi la nchi saba tajiri duniani, G7 walitaka washiriki kukosoa uvamizi wa Urusi Ukraine jambo ambalo limepingwa na wajumbe wa Urusi na China. 

Urusi ambaye ni mwanachama wa G20 na sio G7 imevielezea vita vyake Ukraine kama operesheni maalum ya kijeshi na kuepuka kuviita Uvamizi.