1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoCameroon

Mkutano wa Eto'o na kocha wa Cameroon wageuka kuwa vurugu

28 Mei 2024

Soka nchini Cameroon limetumbukia katika mgogoro mkubwa Jumanne baada ya mkutano kati ya rais wa shirikisho la soka nchini humo Samuel Eto'o na kocha mpya Marc Brys kugeuka kuwa wa kutupiana maneno.

https://p.dw.com/p/4gOGU
Timu ya taifa ya Cameroon
Timu ya taifa ya Cameroon Picha: KENZO TRIBOUILLARD/AFP

Video iliyosambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii na iliyochukuliwa na waandishi wa habari, inamuonyesha Eto'o akimkaribisha kocha huyo mpya wa Cameroon japo baadaye, mkutano huo uligeuka kuwa uwanja wa kurushiana cheche za maneno.

Huo ulikuwa ni mkutano wa kwanza kati ya Eto'o na Brys ambaye aliteuliwa na wizara ya michezo nchini humo kama kocha wa timu ya taifa bila ya ridhaa kutoka shirikisho la soka la Cameroon. Hatua hiyo inatajwa kuwa chanzo cha mgogoro kati ya wawili hao.

Shirikisho la soka nchini humo FECAFOOT inatarajiwa kutoa taarifa hapo baadaye kuhusu tukio hilo.

FECAFOOT ilielezea nia ya kufanya kazi na Mbelgiji huyo licha ya awali kukosoa uteuzi wake na kuutaja kama uamuzi wa mtu mmoja tu uliochukuliwa na Waziri wa michezo Narcisse Mouelle Kombito.