1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ECOWAS yatafuta njia za kutatua changamoto za kikanda

7 Julai 2024

Mkutano wa kilele wa viongozi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi ECOWAS unafanyika licha ya msukosuko wa kisiasa baada ya viongozi wa kijeshi wa Niger, Mali na Burkina Faso kujiondoa katika Jumuiya hiyo.

https://p.dw.com/p/4hymi
Viongozi wa ECOWAS wakutana Abuja
Viongozi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi ECOWAS wakiongozwa na mwenyekiti wao rais wa Nigeria, Bola Tinubu.Picha: Kola Sulaimon/AFP/Getty Images

Nchi hizo tatu zilitangaza kuunda muungano wa pamoja na hii inaonekana kuwa mtihani mwengine mkubwa kwa ECOWAS waliojitenga nayo mapema mwaka huu.

Tayari Jumuiya hiyo inapambana na vurugu zinazodaiwa kufanywa na makundi ya wanamgambo walio na itikadikali, matatizo ya kifedha, na changamoto ya kulileta pamoja jeshi la kikanda.

Vikosi vya Marekani kuanza kuondoka Niger wikiendi hii

Hadi sasa haijawa wazi ni namna gani Jumuiya hiyo ya ECOWAS itakavyojibu hatua ya mataifa hayo matatu kuunda kwa pamoja muungano wa mataifa ya Sahel katika mkutano wao uliofanyika katika mji mkuu wa Niger Niamey jana Jumamosi. 

Mkutano wa ECOWAS pamoja na mambo mengine utajadili kuhusu namna ya kupambana na ugaidi, masuala ya ulinzi, uchumi na biashara.