1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa Berlin kuhusu Libya mwakani

25 Novemba 2019

Mkutano wa kilele uliokuwa ufanyike mjini Berlin, Ujerumani kusaidia kutuliza mzozo nchini Libya, huenda ukafanyika mwanzoni mwa mwaka ujao.

https://p.dw.com/p/3TgR8
Libyen Heiko Maas und Taher Siala
Picha: AFP/M. Turkia

Katika ziara yake nchini Libya mwishoni mwa mwezi Oktoba, Waziri wa Mambo ya kigeni wa Ujerumani, Heiko Maas alielezea matumaini yake kwamba mkutano huo wa kilele utafanyika mwaka huu. 

Libya ilitumbukia katika machafuko tangu kuondolewa madarakani kiongozi wake wa muda mrefu Moamar Gaddafi mwaka 2011na tangu wakati huo serikali mbili nchini humo zinawania madaraka huku makundi kadhaa ya wapiganaji yakipambana kuchukua udhibiti wa mji mkuu, Tripoli.

Tangu mwezi Septemba, Ujerumani imekuwa ikijaribu kuwa mpatanishi katika mzozo wa Libya, kwa matumaini ya kuzuia kuibuka vita kama vya Syria.