1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MKUTANO KATI YA CHAMA-TAWALA SPD NA VIONGOZI WA VYAMA VYA WAFANYIKAZI-BIMA YA KUWATUNZA WAZEE NDIO MADA KUU ZILIZOCHAMBULIWA NA WAHARIRIRI WA MAGAZETI YA LEO YA UJERUMANI:

Ramadhan Ali6 Julai 2004
https://p.dw.com/p/CHQ3

GAZETINI: 06-07-04

Wahariri wa magazeti ya ujerumani leo wameuchambua zaidi mkutano kati ya viongozi wa chama-tawala cha SPD na wa Shirikisho la vyama vya Wafanyikazi-jinsi ya kugharimia bima ya kuwatunza wazee na hali ya fedha ilivyo humu nchini.

Gazeti la kibiashara linalochapishwa mjini Düsseldorf-HANDELSBLATT kuhusu mkutano wa jana kati ya chama cha SPD na shirikisho la vyama vya wafanyikazi DGB laandika:

"Shirikisho hilo la vyama vya wafanyikazi lilikua la kupigiwa mfano hapo zamani.Daraja yake ya hali ya juu ya kuwaongoza wafanyikazi ilivivutia sana vyama vya wafanyikazi vya nchi nyengine.Mzinduko wake wa kuwa na dhamana katika kutochukua hatua zitakazopelekea kudhuru uchumi wa nchi hii zilihusudiwa na waajiri tangu humu nchini hata n’gambo.

Hiyo lakini ni hekaya iliopita zamani.Leo hii , hakuna anaeviheshimu vyama vya wafanyikazi kama VERDI na IG METALL pamoja na shirikisho lao kuu la DGB.Kinyume chake,vyama hivyo vinaachwa mkono na wafuasi wao na chama chao-mshirika wa desturi SPD pia kinavipa mgongo. Lawama ya hali hii yaangukia mabegani ya vyama vya wafanyikazi binafsi humu nchini.Vinawalipa mishahara minono viongozi wa hadhi ya juu ambao wanajifanya vipofu kutozitambua ishara za hali ya uchumi za wakati huu.Kile kinachofanywa na viongozi hawa-Bsirske,Peters na Sommer inatukumbusha uasi wa wafanyikazi uliokandamizwa bila kuleta tija yoyote-Weberaufstand.

Katika gazeti la Braunschweiger Zeitung tunasoma haya:

"Chama-tawala cha SPD kikivutwa huku na kule baina ya wapendao mageuzi na wapinga-mageuzi kinaikokota jahazi lake linaloenda mrama likizidi kupungukiwa na mabaharia katika dharuba ya mawimbi makali baharini na bila kuiona bandari.bandari chombo chao kinachotaka kuifikia ni kutoa nafasi zaidi za kazi na kuleta haki na usawa katika jamii-ni shabaha inayokumbukwa tu.Ukweli wa mambo ni kitambo matanga ya jahazi hilo yamekosa upepo.Vyama vya wafanyikazi hawana kipya ,hawana mkakati imara isipokua ahadi za maneno matupu.Ahadi kama hizo ndio zatia moyo wanachama lakini hazileti upepo mpya kuvuma kukitoa chombo c hao kutoka dharuba hii inayovuma baharini.

kutia munda mageuzi kunaongoza katika hali ya kuzorota mambo sawa na ilivyokua katika sekta ya sera za kijamii wakati wa enzi ya utawala wa Helmut Kohl."

Hilo lilikua BRAUNSCHWEIGER ZEITUNG.

Ama gazeti la OSTSEE linalochapioshwa mjini Rostock lakumbusha kwamba panapozuka shaka shaka ndipo ufa unapoaanza kuingia na kuonekana kati ya wale wapendao kugeuza na wale wanaotaka kuseleleza yaliokuwapo tena katika jamii nzima.Vyama vya wafanyikazi vinashikilia kuseleleza matunda yaliovunwa miaka ya nyuma ingawa msingi wa dola inayowatunza wanyonge kwa mtindo kama huo wa kushikilia pale pale,unamungunyuka........"

Likitubadilishia mada,gazeti la COBURGER TAGEBLATT laandika:

"haja ya kufanya mageuzi katika bima ya kuwatunza wazee inadharauliwa kwa aina ambayo,serikali haingediriki kufanya hivyo katika bima ya afya na ya pencheni.Labda kwa kuwa hapa wanaoathirika hawana nguvu za kujitetea-wakongwe na wagonjwa wasio na sauti. na kwa kuwa mtu anajua kutengeza mambo kuwa bora kunagharimu fedha ambazo hazipo au mtu hataki kuzitoa.

Gazeti la STUTTGARTER NACHRICHTEN laandika:

"Mageuzi halisi na ya kweli yanabidi kufanywa.Bima ya kuwatunza wazee inaathirika kutokana na dhara ilizopata ilipozaliwa.Inadhurika haraka mbele ya matatizo ya jamii inayozidi kukonga.

Serikali ya Muungano wa chama cha SPD na walinzi-mazingira -KIJANI haiombwi makuu isioweza kuyatimiza.Kuigeuza bima ya kuwatunza wazee kunahitajika mifumo ya aina tatu:Yote 3 ni barabara.Lakini hakuna kinachotendeka na kwanini ?

Jibu ni kuwa –serikali hii ya muungano haina nguvu.Kwavile Bunge la pili la serikali za mikoa-Bundesrat laweza kutumia kura yake veto,serikali ya muungano wa chama cha SPD na Kijani inapaswa kuridhiana na muungano wa upinzani wa vyama vya CDU/CSU vyene sauti zaidi katika bunge hilo.Na kwavile hadi mwaka 2006 haiyumkiniki aasilani,hakuna matumaini ya wingu lililotanda kupambazuka.