1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UfisadiUhispania

Mke wa Sanchez atoa ushahidi wa rushwa kwenye biashara zake

5 Julai 2024

Mke wa Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez, Begona Gomez leo atatowa ushahidi mbele ya jaji katika sehemu ya mwanzo ya uchunguzi kuhusu kuwepo ufisadi kwenye shughuli za biashara zake.

https://p.dw.com/p/4huF9
Granada Uhispania | Waziri Mkuu wa Uhispania Sanchez na mkewe Begoña Gomez
Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez akiwa na mkewe Begona Gomez. Mke wa Sanchez ameanza kutoa ushahidi wa kesi ya ufisadi kwenye biashara zake Picha: Álex Cámara/dp/a/Europapresspicture alliance

Kesi hiyo ya ufisadi kwa kiasi kikubwa ilimkasirisha waziri mkuu Sanchez.

Mahakama ya mjini Madrid mwezi uliopita ilimtaka Gomez atoe ushahidi leo Julai 5 kama mtu anayechunguzwa katika uchunguzi huo wa mahakama kuhusiana na tuhuma za ufisadi katika sekta ya binfasi pamoja na ushawishi wa kisiasa.

Kambi ya upinzani ya chama cha mrengo wa kulia imekuwa ikilipalilia suala hili kama ushahidi wao wa tuhuma wanazotowa, kwamba waziri mkuu Sanchez na serikali yake ni mafisadi.

Uchunguzi wa awali ulianzishwa Aprili 16 kufuatia kesi ya malalamiko iliyofunguliwa na shirika moja  lisilokuwa la kiserikali la kupambana na rushwa linaloitwa Manos Limpias ambalo linafungamanishwa na chama cha siasa kali.

Kesi hiyo imemuweka katika hali ngumu waziri mkuu Sanchez ambaye mwishoni mwa mwezi Aprili alitangaza kufikiria kujiuzulu kufuatia kile alichokiita kampeni ya kumdhalilisha kisiasa inayofanywa na vyama vya  mrengo wa kulia.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW