1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNamibia

Mke wa Biden azuru Namibia kama sehemu ya ziara yake Afrika

23 Februari 2023

Jill Biden, ambaye ni mkewe rais wa Marekani Joe Biden, amewasili Namibia, katika ziara yake ya siku tano barani Afrika.

https://p.dw.com/p/4Nry2
US-Midterm - Jill Biden
Picha: Jacquelyn Martin/AP/picture alliance

Jill Biden, ambaye ni mkewe rais wa Marekani Joe Biden, amewasili Namibia, katika ziara yake ya siku tano barani Afrika.

Hii ni mara ya kwanza kwa Jill Biden kuzuru Afrika kama mke wa rais wa Marekani.

Baada ya Namibia, Jill Biden anatarajiwa kuzuru Kenya. Ataangazia suala la kuwawezesha wanawake na vijana Pamoja na tatizo la uhaba wa chakula katika upembe wa Afrika.

Utawala wa Biden unapanga mifululizo ya ziara za maafisa wa ngazi ya juu barani Afrika mwaka huu, kwa lengo la kukabili ushawishi wa Urusi na China katika bara la Afrika.

Ziara ya Jill Biden nchini Namibia imejiri mnamo wakati nchi Jirani Afrika Kusini ni mwenyeji wa luteka ya kijeshi inayoshirikisha Urusi na China.