Mkasa wa kuzama kwa meli Zanzibar: Serikali kuchukua hatua kali dhidi ya uzembe
12 Septemba 2011Matangazo
Kikosi cha wazamiaji 12 kutoka Afrika Kusini ´kimewasili visiwani Zanzibar kusaidia kutafuta maiti za watu takriban 200 waliozama ndani ya meli mapema Jumamosi iliyopita. Matumaini ya kuweza kuwaokoa watu zaidi kufuatia ajali ya meli huko Zanzibar yamefifia.
Wakati huo huo, serikali ya Zanzibar imeapa kwamba itachukuwa hatua zinazostahiki kwa wale wote watakaobainika kufanya uzembe katika mkasa wa kuzama kwa meli hii.
Mwandishi: Josephat Charo
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman