1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mjumbe wa UN kwa Libya: Uchaguzi unawezekana

Josephat Charo
17 Oktoba 2023

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Libya, Abdoulaye Bathily amesema tume ya uchaguzi ya nchi hiyo imemuambia inaweza kuanza maandalizi kuelekea uchaguzi baada ya suala la kuunda serikali mpya kutatuliwa.

https://p.dw.com/p/4Xctq
Libyen Tripolis | UN-Sonderbeauftragter für Libyen Abdoulaye Bathily
Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Libya, Abdoulaye Bathily.Picha: Yousef Murad/AP Photo/picture alliance

Mkwamo kati ya pande hasimu za kisiasa na makundi ya waasi kuhusu serikali ya mpito umeshuhudiwa tangu mapema mwaka uliopita, hali ambayo imeibua mapigano ya mara kwa mara.

Soma zaidi: Mjumbe wa UN asema uthabiti wa Libya umo mashakani

Bathilya alikwa akizungumza mbele ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa baad ya spika wa bunge la Libya mashariki kutangaza sheria mpya za uchaguzi kwa kuzingatia muongozo wa diplomasia ya kimatiafa unaolenga kuutanzua mgogoro wa miaka mingi kupitia uchaguzi.

Soma zaidi: Umoja wa Mataifa waonya kuhusu machafuko Libya

Bathily amesema uchaguzi wa Libya unahitaji serikali imara yenye umoja itakayokubaliwa na wadau wakuu wa mashariki na magharibi ambao kufikia sasa wameonesha ari ndogo kuafikiana.