1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mjumbe wa Umoja wa Ulaya ailaumu Sudan kuwahujumu raia wa kawaida kwa mabomu huko Darfour

13 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDCf

Khartoum:

Mjumbe maalum wa Umoja wa Ulaya PEKKA HAAVISTO ameituhumu serikali ya Sudan kuwashambulia kwa mabomu rais wasioweza kujitetea wa Darfour.Bwana Haavisto anasema akiwa ziarani jimboni Darfour amewaona watoto wadogo waliopata pata majaraha kutokana na mashambulio ya mabomu.Hali ya mambo inakumbusha ile ya mwaka 2003, mapambano yaliporipuka kati ya vikosi vya serikali,wanamgambo wa Djandjawid wanaowaunga mkono na waasi.Zaidi ya watu laki mbili wanasemekana wameuwawa tangu wakati huo.