1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mji wa kihistoria wa Timbuktu wazingirwa na wanamgambo

22 Agosti 2023

Kulingana na maafisa, wapiganaji wa itikadi kali ya dini ya kiislamu wameuzingira mji huo na kuweka vizuizi vikali vya kuingia na kutoka eneo hilo.

https://p.dw.com/p/4VQU7
Mji wa Timbuktu ni sehemu ya maeneo yanayokumbwa na ukosefu wa usalama nchini Mali tangu kuzuka kwa uasi wa itakadi kali mnamo mwaka 2012. (Picha ya maktaba)
Mji wa Timbuktu ni sehemu ya maeneo yanayokumbwa na ukosefu wa usalama nchini Mali tangu kuzuka kwa uasi wa itakadi kali mnamo mwaka 2012. (Picha ya maktaba)Picha: KENZO TRIBOUILLARD/AFP/Getty Images

Maafisa kwenye mji wa kale na wa kihistoria wa Timbuktu uliopo nchini Mali wamesema wapiganaji wa itikadi kali ya dini ya kiislamu wameuzingira mji huo na kuweka vizuizi vikali vya kuingia na kutoka eneo hilo.

Mbunge mmoja wa mji huo aliyezungumza kwa sharti la kutatajwa jina, ameliambia shirika la habari la AFP kuwa wanamgambo "wamezuia barabara zote za mji wa Timbuktu" na hakuna kinachoruhusiwa kutoka wala kuingia kwenye eneo hilo.

Afisa mwingine wa serikali ya mji huo wa kaskazini mwa Mali amesema bei za vitu zimepanda wa sababu hakuna bidhaa inayoruhusiwa kuingia Timbuktu.

Mapema mwezi huu kundi moja la itikadi kali lenye mafungamano na Al-Qaeda lilitoa ujumbe wa kile ilikitaja "kutangaza vita vya kuwania mji huo" na kuwaonya maderava wa malori kutoka nchi za Mauritania, Algeria na kwengine kutoingia kwenye mji huo.

Mji huo ni sehemu ya maeneo yanayokumbwa na ukosefu wa usalama nchini Mali tangu kuzuka kwa uasi wa itakadi kali mnamo mwaka 2012.