1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mji wa Kherson watangaza amri ya kutotembea nje kwa saa 58

3 Mei 2023

Mji wa Kherson ulioko karibu na eneo la mapambano kusini mwa Ukraine, umetangaza amri ya kutotoka nje kwa saa 58 kuanzia Ijumaa jioni

https://p.dw.com/p/4Qpjf
Ukraine Cherson | Angriff auf Bushaltestelle
Picha: Nina Lyashonok/Avalon/Photoshot/picture alliance

Hayo yameelezwa leo na mkuu wa utawala wa kijeshi wa Kherson, Oleksandr Prokudin, wakati ambapo vikosi vya Ukraine vikijiandaa na mashambulizi ya kupambana na vikosi vya Urusi majira ya machipuko.

Katika mtandao wa Telegram, Produkin amesema katika muda huo, ni marufuku watu kutembea kwenye mji huo. Aidha, raia watatu wameuawa katika shambulizi la Urusi lililotokea leo kwenye soko kubwa katika mji wa Kherson.

Wakati huo huo, Idara ya Usalama ya Shirikisho la Urusi, FSB, imesema kuwa watu saba wanaohusishwa na shirika la kijasusi la Ukraine wamekamatwa katika jimbo la Crimea.

FSB imesema mashambulizi dhidi ya Sergei Aksyonov gavana wa jimbo hilo linaloungwa mkono na Urusi, pamoja na maafisa wengine, yamezimwa.