1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mjadala wa muswada wa uraia kwa wanasiasa Congo

9 Julai 2021

Wabunge nchini Congo wamegawanyika kuhusu muswada wa sheria utakaoimarisha vigezo vya uraia kwa wanasiasa wanaotaka kuwania kiiti cha urais. Muswada umependekezwa mgombwa wa zamani wa urais Noël Tshiani Mwadiamvita

https://p.dw.com/p/3wHkq
Senat in Kinshasa, Demokratische Republik Kongo
Picha: AFP/Getty Images/J. D. Kannah

Muswada huo uliopendekezwa na aliyewahi kuwa mgombea wa kiti cha urais Noël Tshiani Mwadiamvita, unataka wagombea wa kiti cha urais wawe raia wa wanasiasa ambao wazazi wote wawili ni raia wa Congo.

Muswada huo unaoitwa "sheria ya Tshiani" umekuwa kitovu cha gumzo tangu ulipowasilishwa bungeni hivi karibuni hapa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Iwapo itapitishwa sheria mpya itaruhusu Wakongomani kuwa na uraia zaidi ya mmoja, wakati ikiweka masharti makali kwa wale wanaotaka kuwani wadhifa wa rais wa jamhuri. Yaani, kulingana na mapendekezo ya Tshiani, ni Wakongomani tu waliozaliwa na wazazi walio raia kamili wa Congo ndiyo waruhusiwe kugombea urais wa nchi hii.

Moise Katumbi kongolesischer Oppositionsführer
Mama wa Katumbi ni Mkongo na baba ni MgirikiPicha: picture-alliance/Keystone/M. Trezzini

Lengo ni kulinda utaifa kama alivyoeleza Singi Pululu, mubunge aliyeufikisha  muswada huo bungeni.

((Tulitambua michanganyiko ya uraia tangu mwaka 1964 na tuliona kwamba swala hilo la uraia linarejea na kutafuta suluhisho. Halafu leo naona nisipowasilisha muswada huu ni makosa kwangu. Ni muhimu kila mtu ambae baba na mama ni wakongomani aunge mkono. Ni kwa faida ya wote.))

Muswada huu umewagawanya wabunge, ambao baadhi yao wanawaza ni sheria ya mgawanyiko ambayo inaweza kusababisha machafuko hapa nyumbani, kama ilivyowahi kujitokeza katika nchi zingine.

Miongoni mwa wabunge wanaopinga kutungwa kwa sheria hiyo ni Juvenal Munubo toka chama cha UNC, akiamini kuwa sio kipaumbele kwa Wakongomani.

((Kile watu wanaomba leo ni amani irudi mashariki mwa Kongo, Amani irudi kote Nchini na watu wapate chakula, wapate maji safi, wapate umeme, wajenge barabara. ndiyo kile watu wanahitaji rais afanye.  Nchi nyingine zilijaribu mipango kama hiyo na haikuleta amani hiyo haikuleta amani.))

Baadhi ya wachambuzi wanawaza  kwamba muswada huu ulianzishwa ili kujaribu kumwondoa kwenye uchaguzi wa urais wa 2023, Moïse Katumbi ambaye kwa sasa, anaonekana kuwa mgombea mwenye nguvu.  Katumbi ni raia wa Congo lakini babake ni Mgiriki.

Jean Noël Ba-Mweze, DW, Kinshasa