Mjadala wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
24 Septemba 2009NEW YORK:
Rais Barack Obama wa Marekani ametoa
mwito juu ya kusimama pamoja katika
kuzikabili changamoto kubwa za dunia.
Akilihutubia Baraza Kuu ya Umoja wa Mataifa kwa mara ya kwanza tokea aingie madarakani, Obama amesema jumuiya ya kimataifa inapaswa kushirikiana katika kuzikabili changamoto hizo.
Amesema Marekani peke yake haitaweza kutatua matatizo yote ya dunia. Amezitaka nchi ambazo zimekuwa zinaikosoa Marekani kwa kupitisha maamuzi pake yake , sasa kutosimama kando wakati Marekani ikitatua matatizo. Amesema wakati sasa umefika kwa wote kutimiza wajibu wao.
Rais Obama amezitaja changamoto zinazoikabili dunia kuwa pamoja na hatari ya silaha za nyuklia, vita, tishio linalotokana na mabadiliko ya hali ya hewa na mgogoro wa uchumi.