1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Misri yawasilisha juhudi kumaliza mzozo Libya

Sekione Kitojo
6 Juni 2020

Rais wa  Misri Abel-Fattah al-Sissi  ametangaza juhudi za  kumaliza mzozo  katika  nchi  jirani  ya  Libya, ikiwa  ni  pamoja  na mapendekezo  ya  kusitisha  mapigano yatakayoanza  rasmi Jumatatu (08.06.2020).

https://p.dw.com/p/3dLS7
Symbolbild Ägypten Präsident Abdel-Fattah el-Sissi
Picha: picture-alliance/AP Photo/MENA

Kiongozi  huyo  wa  Misri  amewasilisha  juhudi  hiyo  mjini  Cairo akiwa  pamoja  na  kamanda  Khalifa Haftar, mkuu  wa  jeshi linalojiita  jeshi  la  taifa  la  Libya.

Deutschland Berlin | Libyen Krieg | General Chalifa Haftar
Jenerali Khalifa Haftar akiwa mjini Berlin alikohudhuria mazungumzo ya kusitisha mapigano nchini mwake yaliyandaliwa na UjerumaniPicha: Getty Images/S. Gallup

Pendekezo hilo la  juhudi  linatoa  wito wa kuondoka  kwa wanamgambo wa  kigeni  kutoka  Libya, ikiwa  na  maana  ya wapignaji  mamluki wanaodaiwa  kuingizwa  nchini  humo  na  Uturuki wakisaidia  mahasimu  wa  Haftar.

Wanajeshi  watiifu  kwa  Haftar wamepata  wamepata hasara kubwa kijeshi dhidi  ya  majeshi  yenye  mafungamano  na  serikali ya makubaliano ya kitaifa  GNA inayoungwa  mkono  na  Umoja  wa mataifa  na  yenye  makao  yake mjini Tripoli.

Rais Abdel-Fattah el-Sissi  alitangaza  juhudi  hizo  katika  sherehe mjini  Cairo  iliyohudhuriwa  na  kamanda  Haftar  pamoja  na  Aguila Saleh , spika  wa  baraza  la  wawakilishi  linalofanya  shughuli  zake Tobruk. El-Sissi  amesema  juhudi  hizo, ambazo zinajumuisha kusitisha  mapigano , zina  lenga  ksafisha  njia  kwa  ajili  ya uchaguzi  katika  taifa  hilo  lenye  utajiri  wa  mafuta.

Hakuna maelezo  ya  mara  moja  kutoka  katika  serikali inayoungwa  mkono  na  Umoja  wa  mataifa  katika  mji  mkuu Tripoli.

Libyen Truppen von General Haftar zurückgedrängt
Wapiganaji wenye mafungamano na serikali inayotambuliwa na Umoja wa mataifa wakisherehekea ushindi katika mji wa Tarhouna, mashariki mwa Tripoli.Picha: Getty Images/AFP/M. Turkia

Jeshi  la  Haftar

Jeshi  la  Haftar  linalojulikana  kama  Libyan Arab Armed  Forces lililoko  upande  wa  mashariki lilianzisha  mashambulizi  mwaka ulipita  kuukamata  mji  mkuu  Tripoli. Lakini  hivi  karibuni  amepoteza maeneo  muhimu  ya  kimkakati magharibi  mwa  Libya  baada  ya Uturuki kuongeza  msaada  wake  kwa  makundi  kadhaa  ya wanamgambo ambayo yanamafungamano  na  serikali  yenye makao  yake  makuu  mjini  Tripoli.

Majeshi  ya  Haftar yanaungwa  mkono  na  Ufaransa, Urusi, Jordan , Umoja  wa  Falme  za  Kiarabu  pamoja  na  washirika  wengine muhimu  katika  mataifa  ya  Kiarabu.

Libyen Symbolbild LNA
Majeshi ya kamanda Khalifa Haftar katika mashambuliz dhidi ya mji wa TripoliPicha: Reuters/Esam Omran Al-Fetori

Pamoja  na  Uturuki, serikali  mjini  Tripoli  inaungwa  mkono  na italia  na  Qatar. Libya  imekuwa  katika  machafuko  tangu  mwaka 2011 wakati  vita  vya  wenyewe  kwa  wenyewe  viliposababishwa kuangushwa  kwa  utawala wa  kiongozi  wa  muda  mrefu  Moammar Gaddafi, ambaye  baadaye  aliuwawa.

Nchi  hiyo  imegawanyika  katika  serikali  hasimu  upande  wa mashariki  na  magharibi, kila  moja  ikiungwa  mkono na  makundi yenye  silaha pamoja  na  serikali  za  kigeni.