1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Misri yawarejesha makwao maelfu ya wakimbizi wa Sudan

19 Juni 2024

Shirika la haki za binaadamu la Amnesty International limesema Misri imewakamata na kuwarudisha makwao kinyume cha sheria maelfu ya wakimbizi wanaokimbia vita nchini Sudan.

https://p.dw.com/p/4hGbU
Wakimbizi wa Sudan
Baadhi ya wakimbizi wa Sudan wakiwa mjini Kairo, Misri.Picha: Khaled Elfiqi/Matrix Images/picture alliance

Shirika hilo lilisema lina ushahidi wa matukio 12 ambapo mamlaka za Misri ziliwarudisha makwao jumla ya raia 800 wa Sudan kati ya Januari na Machi mwaka huu, bila ya kuwapa fursa ya kuomba hifadhi au kupinga maamuzi ya kuwarudisha makwao.

Soma zaidi: IOM: Idadi ya wakimbizi wa ndani Sudan yapindukia watu milioni 10

Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) linasema maelfu walirudishwa mwaka jana.

Idara ya Huduma ya Mawasiliano ya Kitaifa nchini Misri haikupatikana kuzungumzia madai hayo.