1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Milio ya risasi imerindima Sudan

25 Aprili 2023

Milio ya risasi imerindima leo katika maeneo ya mji mkuu wa Sudan, Khartoum licha ya kuwepo makubaliano yaliyosimamiwa na Marekani kati ya majenerali wawili wanaozozana ya kusitisha mapigano kwa saa 72

https://p.dw.com/p/4QWdA
Sudan | Kämpfe in Khartum
Picha: AFP/Getty Images

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Antony Blinken aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa Jeshi la Sudan na kikosi cha msaada wa dharura - RSF walikubaliana kuweka chini silaha baada ya mazungumzo yaliyofikiwa jana usiku. Majaribio ya awali ya kusitisha mapigano kwa muda hayakuheshimiwa, lakini mara hii pande hizo mbili zimethibitisha kuwa zimekubaliana kuweka chini silaha kwa siku tatu. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameonya kuwa Sudan iko kwenye ukingo wa kuangamia.Hayo ni wakati nchi za kigeni zikiendelea kuwaondoa raia wake walionaswa katika mgogoro huo.