MILAN: Silvio Berlusconi azimia kwenye mkutano wa hadhara
26 Novemba 2006Matangazo
Waziri mkuu wa zamani wa Italia,Silvio Berlusconi alizimia wakati wa kuhotubia mkutano wa hadhara kaskazini mwa nchi.Ripoti zinasema sasa anapumzika nyumbani kwake karibu na mji wa Milan alikopelekwa kwa helikopta.Berlusconi,anaeongoza chama cha upinzani chenye sera za wastani za mrengo wa kulia tangu kushindwa uchaguzi mwezi wa Aprili,alionekana kwenye televisheni akizimia mikononi mwa wasaidizi wake alipokuwa akihotubia wafuasi wake katika mji wa Montecatini Terme, karibu na Florence.Berlusconi ni miongoni mwa watu tajiri kabisa nchini Italia na anadhibiti kundi kubwa la vyombo vya habari.Juma lililopita alifikishwa mahakamani kwa tuhuma za kufanya udanganyifu na kuhamisha pesa zisizo halali.