1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mikutano ya kilele ya G-8 na NATO huko Marekani

21 Mei 2012

Mkutano wa kilele wa mataifa 8 tajiri -G-8 huko Camp David na ule wa jumuia ya kujihami mjini Chicago na uchaguzi wa rais nchini Misri ni miongoni mwa yaliyoochambuliwa na wahariri wa magazeti ya Ujerumani .

https://p.dw.com/p/14zJD
Viongozi wa mataifa tajiri kiviwanda katika karamu iliyoandaliwa na mwenyeji wao rais Barak Obama wa MarekaniPicha: dapd

Tuanzie lakini Marekani ambako mkutano wa viongozi wa mataifa saba tajiri kiviwanda na Urusi-G-8 umemalizika huko Camp David na kila mmoja ameridhika kwa upande wake.Gazeti la "Neue Presse la mjini Hannover linaandika:Kazi zaidi,ukuaji zaidi wa kiuchumi,matumizi yazidi kupunguzwa na nakisi ya bajeti ipunguzwe-hizo ndizo fikra ambazo viongozi wa kundi la G-8 walikubaliana nazo katika mkutano wao huko Camp David.Tafsiri ya taarifa ya mwisho ya mkutano huo ni bayana:bora kila mmoja aridhike,muhimu watu hawagombani.Maneno matupu hayawasaidii hata kidogo wananchi nchini Ugiriki,Hispania,Italy au Ufaransa.Jumatano ijayo viongozi wa Umoja wa ulaya watakutana mjini Brussels.Hapo hali halisi ya mambo itabidi ijadiliwe.

Gazeti la "Stuttgarter Nachrichten" linazungumzia zaidi jinsi wananchi wanavyochoshwa naa kuandika:Watu wamechoshwa na hadaa na mivutano kati ya mwenye kupigania hatua za kufunga mkaja,yaani kansela Angela Merkel na wawakilishi wa mpango wa kutolewa mikopo ili kuhimiza ukuaji wa kiuchumi:Kufumba na kufumbua sasa watu wamefikia maridhiano kwa namna ambayo kila mmoja kati ya washirika wa mkutano wa kilele wa G-8 anarejea nyumbani kifua mbele na kuendelea kufuata msimamo wake madarakani au kuutumia katika kampeni za uchaguzi.Lakini tatizo limesalia pale pale-halijapatiwa ufumbuzi.

Auftakt G8-Gipfel in Camp David (USA)
Kansela Angela Merkel na waziri mkuu wa Urusi Dmitri MedvedevPicha: dapd

Mbali na mkutano wa kilele wa Camp David,wahariri wamejishughulisha pia na ule wa jumuia ya kujihami ya NATO huko Chicago.Na gazeti la "Dresdner Neueste Nachrichten" linajiuliza:"NATO unaelekea wapi na nani wa kugharimia shughuli zote hizo?Masuala haya ndiyo yatakayojadiliwa kwa kina katika mkutano wa kilele wa Chicago.Ikizongwa na mitihani ya kila aina kuanzia masilahi yasiyo lingana,makasha matupu na ukosefu wa motisha,jumuia hiyo ya kujihami iliyodumu zaidi ya miaka 60 inatafakari.Jukumu kubwa la NATO katika eneo la Balkan na Afghanistan linakurubia kumalizika-matokeo yake ni dhaifu.Afghanistan haiko katika njiani kuelekea mfumo wa kidemokrasi na eneo la Balkan bado halijajipatia utulivu wa kudumu.Na baada ya rais mpya wa Ufaransa Francois Hollande kuahidi katika kampeni yake ya uchaguzi,wanajeshi wa nchi hiyo walioko Afghanistan watarejea nyumbani hadi ifikapo mwisho wa mwaka huu,NATO inabidi itahadhari kila mmoja asije akataka kufuata njia hiyo ya mkato.

NATO-Gipfel in Chicago 2012
Kansela Merkel katika mkutano wa kilele wa Chicago akizungumza na rais Obama (kulia) na katibu mkuu wa NATO Andres Fogh RasmussenPicha: picture-alliance/dpa

Mada ya mwisho magazetini hii leo inahusiana na uchaguzi wa rais nchini Misri.Gazeti la "Süddeutsche Zeitung" linaandika: Orodha ya wagombea haiambatani na umuhimu wa uchaguzi huu wa kwanza huru baada ya kutimuliwa madarakani Hosni Mubarak.Hakuna mgombea yeyote aliyejitokeza na mpango madhubuti kujibu kilio cha wanamapinduzi waliokusanyika mkatika uwanja wa Tahrir.Hakuna anaeonyesha moyo wa kutaka mageuzi,masikilizano,uzoefu na uwezo.Hakuna aliyeonyesha jinsi anavyopanga kuyaúnganisha makundi ya jamii yanayohitilafiana.Hata vijana wana mapinduzi na upande wa upinzani wanavunja moyo.Hawakufanikiwa hata kumteuwa mgombea ambae angalao angeyapa sura madai yao.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Inlandspresse

Mhariri Yusuf Saumu